Breaking News

MATOKEO Ya Simba Vs Bravos do Maquis Leo Tarehe (27 November 2024)

MATOKEO Ya Simba Vs Bravos do Maquis Leo Tarehe 27 November 2024

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kuanza vizuri baada ya kuifunga FC Bravos kutoka nchini Angola bao 1-0, katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba inakwenda kileleni katika msimamo wa kundi wakisubiri mchezo kati ya CS Sfaxien dhidi ya CS Constantine ya Algeria utakaopigwa majira ya saa 1:00 usiku.

Baada ya kupata ushindi huo Simba wataanza kujiandaa kuelekea mchezo wao wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Singida Black Stars, mchezo utakaopigwa pale CCM Liti mkoani Singida, Desemba Mosi, 2024.

Desemba nane Simba atarejea kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo watafunga safari mpaka Algeria kuwakabili CS Constantine.

No comments