Hot Widget

Type Here to Get Search Results !

Zuchu Kulipa Billion 10 Kuondoka WCB

 Mbunge na Mlezi wa WCB ametangaza kupitia ukurasa wake wa instagram kwamba lebo ya Diamond inatarajia kutambulisha wasanii wawili watakaosainiwa hivi karibuni ila akaongezea kwa kusema kwamba safari msanii atakuwa na mashahidi wawili kutoka COSOTA na BASATA.

Miongoni yaliyoibuka katika post hiyo iliyowekwa instagram zilimiminika Comments za wadau mbalimbali na miongoni mwa walioandika ni Diamond Platnumz ambae yeye alicomment na kuandika “Mnataka mkawanyonye watu wengine eeh?.

Baada ya comment hiyo ya Diamond ziliibuka comments nyingi za mashabiki ikiwemo ya shabiki aliyemuuliza  Diamond kwamba Kama Zuchu nae akitaka kuondoka WCB anatakiwa kulipa kiasi gani cha pesa, 

Diamond alikuwa anamjibu shabiki aliyemuuliza Zuchu angelipa pesa ngapi.

" aahh huyo si chini ya 10 billion si unaona manamba yake huko mjini Youtube baba," Alisema Diamond.

Huku Zuchu akijibu matamshi ya bosi wake alisema;

"Msanii anapoamua kubaki au kuondoka kwenye lebo naamini kila mkataba una makubaliano yanayopendelea pande zote mbili,Ulikaa na kukubaliana, ikiwa ni shimo uliloingia ulichimba hela mwenyewe."

Aliongeza kuwa;

"Ikiwa kuna mambo ulitaka yabadilishwe ulikuwa na nafasi ya kufanya hivyo mwenyewe.Kila kitu kinajadiliwa,Wasanii walikuwa wanaondoka WCB hata kabla sijajiunga, kama ingetegemea mambo mengine ningesaini mkataba."

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad